This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/04/18 at 09:43
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Eric J. Shigongo

Eric J. Shigongo

Eric Shigongo ni mfanyabiashara, mjasiriamali, mwandishi, mtungaji vitabu na mfasiri wa vitabu na hadithi kutoka kiingereza kwenda Kiswahili na mhamasishaji Mtanzania.

Alikuwa pia kiongozi wa Vijana wa CCM aliyegombea na kushindwa katika kura za maoni za uchaguzi wa CCM mwaka 2010.

Kwa mujibu wa TCRA (2018), Global Publishers & General Enterprises Limited inamilikiwa 100% na Joachim Lusana Buyobe. Buyobe pia anamiliki Geita Online TV kwa 100%. Hata hivyo Shigongo pia anaonesha kuhusika kwa karibu na kampuni. Anatajwa kuwa ni Ofisa Mtendaji Mkuu, Mkurugenzi na Msimamizi wa global Group - na wakati mwingine kuwa ni mmiliki wa tovuti nyingi. Aidha anaitaja kampuni kwenye facebook yake. Nafasi yake halisi haifahamiki kwa sababu wasifu wa kampuni yake haupatikani katika Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na kampuni hiyo haikujibu maswali ya mahojiano.

Shigongo alianzisha kampuni pamoja na Abdallah Mrisho Salawi mwaka 1998, na wakati huo ndipo alipoanza kuchapisha riwaya pia. Global Publishers inachapisha magazeti ya wiki ya Uwazi, Ijumaa, ijumaa Wikiendi, Risasi, Amani na Championi yote kwa lugha ya Kiswahili.

Shigongo amepata umaarufu kama mjasiriamali, mtungaji vitabu na msemaji. Amezaliwa Mwanza katika mwambao wa Ziwa Victoria. Ana aina nyingi ya miradi na kampuni, ikiwemo vyombo vya habari, hoteli, kilimo, milki ya ardhi na uendelezaji wa majengo. Yeye ni mwandishi maarufu hasa katika hadithi za mfululizo magazetini na riwaya. Historia yake kama mwandishi inahusiana na shughuli yake katika sekta ya uchapishaji, wakati anapoandika mfululizo wa hadithi kwenye magazeti yake mwenyewe.

Miongoni mwa vitabu vinavyosomwa na kuandikwa na Eric Shigongo ni “Rais Anampenda Mke Wangu” kwa kiingereza “The President Loves My Wife” mwaka (2003), The Last Days of My Life(2001), Tears and Blood na vingine vingi.

Kwa sasa Shigongo anasoma Shahada ya kwanza katika Mawasiliano na Umma (Mass Communication) chuo kikuu cha Tumaini, Ndaki ya Dar es Salaam (TUDARCO).

Kampuni ya vyombo vya Habari
Aina za vyombo vya habari
Halisia

Maelezo ya ziada

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ