This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/04/16 at 20:13
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Joseph M. Kusaga

Joseph M. Kusaga

Joseph Kusaga ni mwanzilishi wa CLOUDS Entertainment Limited, alizaliwa na kulelewa Musoma, mji uliopo kwenye ufukwe wa Ziwa Victoria. Alihamia Dar es salaam akiwa na umri wa miaka 5 baada ya baba yake aliyekuwa mtumishi wa serikali kuhamishiwa kwenye jiji la biashara. Yeye ni mtoto wa nne kwenye familia ya watoto tisa, wavulana watano na wasichana wane.

Kusaga alikuwa na shauku ya muziki tangu umri mdogo sana. Alianza kuandaa matamasha tangu alipokuwa chuoni akisomea Electronics. Ingawa Baba na Mama yake hawakuwa na matumaini makubwa katika kuandaa matamasha, walimwamini na kuwa na uhakika nae, na hatimaye, kwa msaada wa wazazi, na baada ya kipindi kifupi alikuwa DJ maarufu na mtayarishaji matamasha.

Alipata wazo la kuanzisha kampuni ya vyombo vya habari wakati wa ziara yake nchini Marekani alipoishi New York City na Los Angeles na kuvutiwa na hali ya muziki wa sehemu hiyo. Alipokuwa Los Angeles aliungana na mbia mwenzake wa biashara wa muda mrefu Ruge Mutahaba na kuanzisha mpango wa kufungua kituo cha redio nchini Tanzania ambacho kitajulikana kuwa ni CLOUDS FM.

CLOUDS-ambacho ni kifupisho cha Cool, Lovable, Outrageus, Unique, Dynamic, Sound ilianzishwa mwaka 1998 nakukua na kuwa miongoni mwa vyombo vya habari maarufu sana nchini Tanzania. Hivi sasa Clouds Entertainment Limited inajumuisha Clouds FM, PrimeTime Promotions, Choice FM, Coconut Radia Station, Clouds TV, Ngoma Web Tv na Kitangoma Magazine.

Upo wasifu wa Clouds Television katika Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ambapo Alex Mkama Kusaga ana (25%) ya hisa, kama alivyo Joseph Kusaga. Clouds Entertainment Limited ina 50% ya hisa. Wamiliki wa sasa wa hisa za Clouds Entertainment ni Joseph Kusaga 50%, Judith Violet kusaga 10%, Sheba Martha Kusaga (10%) Dogan Andrew Kusaga (10%), Joyce Alex Kusaga(10%), Alex Justine Kusaga (5%) na Prisca Mkama Kusaga (10%) .

Uhusiano wa Joseph Kusaga kwa wamiliki wa hisa wa Kusaga bado haufahamiki.

Kampuni ya vyombo vya Habari
Aina za vyombo vya habari
  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ