This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-rsf.org/en/ retrieved on 2022/05/18 at 02:36
Reporters Without Borders (RSF) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Reporters without borders

Sahara Media Group Limited

Sahara Media Group Limited

Sahara Media Group (SMG) iliyokuwa ikiitwa Sahara Communication and Publishing Company Limited ni miongoni mwa kampuni za vyombo vya habari zinazoongoza nchini Tanzania. SMG ilianzishwa mwaka 1992 baada ya biashara huru wakati vyombo vya habari vingi vya binafsi vilipoanza nchini Tanzania. Tangu ilipoanzishwa, Sahara Media Group, yenye makao makuu yake Mwanza, mji mkuu wa pili Tanzania kwenye Ziwa Victoria, imekuwa hadi kuwa miongoni mwa kampuni za vyombo vya habari inayoongoza nchini Tanzania na Africa Mashariki na Kati. Kampuni hiyo inatoa huduma za vyombo vya habari zifuatazo: Matangazo kwa njia ya Televisheni na redio; Matangazo mubashara; Huduma za kukodisha Gari la Matangazo ya Nje; Huduma za matangazo ya TV za kidijiti na matangazo kwa njia ya Satellite.

Kampuni hii ya vyombo vya habari inaendesha Star TV, Radio Free Africa na Kiss FM. Pia iliwahi kuchapisha magazeti ya Kiswahili ya kila wiki (Msanii Africa na Sauti ya Afrika) Weekly mail na Usanii. Hata hivyo yalifungwa kutokana na mauzo madogo.

Mpaka wakati tunaandika habari hizi, data za SMG hazikuweza kupatikana katika Wakala ya Usajili wa Biashara na Utoaji wa Leseni (BRELA). Dr. Anthony Diallo ni miongoni mwa waasisi wa SMG, ni mwanachama wa Chama tawala na kwa sasa ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza. Kwa mujibu wa wasifu wake ulivyounganishwa kwenye mtandao, yeye bado ni Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo tangu mwaka 2010.

Diallo, aliyezaliwa 25 Desemba mwaka 1959, ametoa huduma katika nyadhifa mbalimbali kwenye chama na Serikali. Alikuwa mbunge kuanzia mwaka 1995 hadi 2010. Mpaka mwaka 2008 alikuwa Waziri wa Mifugo pamoja na Maliasili na Utalii, kabla ya kuacha uwaziri ili aweze kuendesha biashara zake zaidi, zinazojumuisha magazeti, na kuimarisha utendaji wa vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa dodoso lilitayarishwa na R &D manager wa SMG, hakuna utafiti uliofanywa kutathmini mapato ya matangazo kwa kila kituo cha FTA. Serikali inaipa kampuni hiyo habari na taarifa, hata hivyo haisaidii sana katika matangazo ya taifa.

Taarifa muhimu

Aina ya Biashara

Binafsi

Mfumo kisheria

Kampuni ya dhima yenye kikomo

Nyanja za Kibiashara

Utangazaji

Umiliki

Mmiliki Binafsi

Dr. Anthony Diallo

Hakuna wasifu wa kampuni BRELA. Wamiliki wa hisa inawezekana wasiwe sahihi. Dialloni mwanasiasa wa CCM na inaelekea kuwan ni muasisi na mmiliki na Ofisa Mtendaji Mkuu

?
Vyombo vya habari
Other Media Outlets

Magazeti mengine

Msanii Afrika (closed)

Televisheni zingine

Star TV

Radio nyingine

Radio Free Africa

Digitali nyingine

registered as a Online Content Service at TCRA.

Halisia

Chombo cha habari cha kibiashara

Broadcasting

Sahara Media Group Limited

Biashara

none

none

Maelezo yote

Mwaka wa kuanzishwa

1992

Mwanzilishi

Dr. Anthony M. Diallo - is a politician and Mwanza Regional Party Chairman of the ruling Chama cha Mapinduzi (CCM). He was a Member of Parliament (1995 to October 2010) when he lost to the opposition candidate. He served in different capacities in the cabinet from 2000 to 2008.

Waajiriwa

204

Mawasiliano

Plot No. 5-7, Ilemela Industrial Area

Airport Road,

P.O Box 1732,

Mwanza

 

Namba ya kutambulika

BRELA incorporation n°: 179974

Taarifa za kifedha

Taarifa ya Kifedha

Taarifa zisizopatikana

Faida za uendeshaji

Taarifa zisizopatikana

Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)

Taarifa zisizopatikana

Utawala

Bodi ya utendaji + Bodi Maslahi ya utendaji

Taarifa zisizopatikana

Bodi isiyo ya utendaji + Bodi maslahi isiyo ya utendaji

Taarifa zisizopatikana

Bodi ya usimamizi + Bodi Maslahi ya usimamizi

Taarifa zisizopatikana

Maelezo ya ziada

Taarifa zisizopatikana

Taarifa za wamiliki wa vyombo vya Habari ambazo hazikupatikana, kampuni zakataa kutoa maelezo au hazikujibu au hazina hifadhi ya kumbukumbu zake

1 ♥

Taarifa ya ziada

No company profile available at BRELA. Registered at TCRA, no shareholders. mentioned. No return of questionnaire.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Reporters without borders
  • Funded by
    BMZ