E FM
E-FM ni kituo cha redio kinachofanyakazi chini ya kampuni mama ya E-FM Company Limited. Ilianza shughuli zake mwaka 2014.
E-FM ni kituo cha redio kinachotangaza saa 24 free to air na kituo cha redio cha biashara chenye makao yake makuu Dar es Salaam, Tanzania. Vipindi vya E-FM vinatangaza masuala mbalimbali kuanzia habari, michezo, matukio, vipindi maalumu (vya nchini na vya kimataifa), mitindo ya maisha, burudani na vinginevyo.
Kama ilivyoelezwa na ripoti ya Tanzania Media Measurement na GeoPoll, kwa takwimu za robo mwaka ya pili ya mwaka 2018, Redio E-FM ni ya tatu kwa idadi ya wasikilizaji XX.XXX% miongoni mwa vituo 20 vya redio nchini Tanzania.
Tehehe 2 Aprili, 2014 E-FM ilianza kutangaza kwa majaribio na kuanza utangazaji rasmi mwaka huo huo, na kuwa redio ya burudani maarufu miongoni mwa wasikilizaji vijana wa Dar es salaam na mikoa mingine 8 nchini.
E-FM Company Limited pia inamiliki kituo cha TV kijulikanacho kama TVE. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na vyanzo vingine, zilionesha kuwa kampuni hii inamilikiwa na ndugu watatu, ambapo Francis Antony Ciza anamiliki 40% ya hisa, Jean Claude Ciza 40% ya hisa na Justine Antoine Ciza anamiliki 20% ya hisa. Wao ni Wanahisa na Wakurugenzi.
Licha ya kuwa miongoni mwa wanahisa na mtendaji mkuu wa E-FM Company Limited, Francis Antony Ciza anamiliki zaidi ya Nigh Club moja zilizopo katika mikoa mbalimbali nchini. Aliwahi kuwa DJ katika redio ya Magic FM.
Isa za hadhira
Aina ya umiliki
binafsi
Maeneo yanayofikiwa
Taifa
Aina ya maudhui
Maudhui huru
Kampuni ya vyombo vya Habari
E-FM Company Limited
Muundo wa umiliki
TV E inaendeshwa na E-FM Company Limited, inayomilikiwa na familia ya Ciza..
Haki ya kuchagua
Taarifa zisizopatikana
Mmiliki Binafsi
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
Start: April 2014 on a trial basis
Mwanzilishi
Justina Antoine Ciza. Francis Antony Ciza. Jean Claude Ciza.
Mtendaji Mkuu
Francis Antony Ciza - anamiliki zaidi ya Night Club Moja kwenye mikoa ya mbalimbali nchini, pia alikuwa DJ wa Magic FM radio.
Mhariri Mkuu
Scholastica Mazula - mwandishi wa habari - Aliwahi kufanyakazi Times Redio
Mawasiliano
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Isa katika soko
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Kiwango cha hadhira kwa mujibu wa ripoti ya viwango vya GeoPoll ya Redio & TV (Aprili – Juni 2018).