This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-rsf.org/en/ retrieved on 2021/10/22 at 06:21
Reporters Without Borders (RSF) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Reporters without borders

Nipashe

Gazeti la NIPASHE ni sehemu ya The Guardian Limited, ambalo pia humilikiwa na IPP Group Limited. The Guardian Limited imeingia kwenye ushindani na Business Times Limited, zamani wakati huo Managing Director Vumi Urassa alizindua NIPASHE mwezi wa Aprili, 1994.

NIPASHE ni gazeti la Kiswahili la kila siku linalolenga wananchi kwa jumla na kuwahudumia makundi ya umri wote na kutoa mchanganyiko wa habari, makala, uchambuzi, picha, siasa, uchumi, elimu, michezo, burudani na masuala mengine. Gazeti hili la kila siku huifikia mikoa yote nchini, na wakazi wa Dar es Salaam ndiyo wasomaji wake wakubwa.

Kwa mujibu wa utafiti wa matumizi ya vyombo vya habari wa GeoPoll (Agost 30 – 1 Sept, 2018), Nipashe ni gazeti la pili maarufu sana lenye XX.XXX% ya wasomaji. Kwa mujibu wa kampuni yenyewe, usambazaji wa Gazeti la NIPASHE ni nakala 28,000 kwa siku, na kila nakala inasemakana kusomwa na takribani watu 10 kwa siku. NIPASHE pia huchapisha gazeti moja la wiki lijulikanalo kuwa NIPASHE, Jumapili.

Kwa mujibu wa utafiti wa ubora wa vyombo vya habari uliofadhiliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), Nipashe inawasilisha habari zenye mitazamo mbalimbali, inamaanisha kuwa mijadala kutoka angalau pande mbili hutumika. Pia makala za Nipashe hueleza vyanzo vya tukio vizuri zaidi na huweka taarifa na takwimu kwa muktadha mzuri. Inafurahisha pia jinsi mara nyingi inaporejea kwa mamlaka au viongozi wakati inapojenga hoja.

- Katika takribani kila habari ya nne, mamlaka au viongozi hutajwa kama chanzo.

NIPASHE inafanyakazi chini ya mwavuli wa The Guardian ambalo ni sehemu ya IPP Group Limited. IPP Group Limited ni kampuni ya utengenezaji, utiaji vinywajio kwenye chupa na kundi la vyombo vya habari inayojumuisha vituo vya Television na redio na magazeti. Wsifu wa Kampuni uliyoombwa kutoka Masjala ya Biashara inaonesha kuwa Dkt. Reginald Abraham Mengi ni mwanahisa wa IPP Group Limited pamoja na Agapitus Leon Nguma.

Mengi alizaliwa Tanzania mwaka 1944, yeye ni mfadhili wa Kitanzania, mwana viwanda mmiliki wa vyombo vya habari na mwasisi na mwenyekiti mtendaji wa IPP Group. Mengi pia ni Makamu wa Rais wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) Tanzania. Katika taarifa za FORBES, amekuwa miongoni mwa matajiri wa Afrika, mwenye zaidi ya $ 400 Milioni, kwa takwimu za mwaka 2015.

Taarifa muhimu

Isa za hadhira

XX.XX%

Aina ya umiliki

Binafsi

Maeneo yanayofikiwa

National (mainland)

Aina ya maudhui

Paid Content

Taarifa zinazopatikana kiurahisi

Upatikanaji wa taarifa za umiliki kutoka kwa vyanzo vingine, kwa mfano vile vinavyotambulikana kisheria

2 ♥

Kampuni ya vyombo vya Habari

IPP Media Limited

Umiliki

Muundo wa umiliki

NIPASHE inaendeshwa chini ya kampuni mama ya The Guardian ambayo ni sehemu ya IPP Group Limited. IPP inamilikiwa na Dr. Reginald Mengi.

Haki ya kuchagua

Taarifa zisizopatikana

Kundi / Mmiliki Binafsi

Taarifa zisizopatikana

Taarifa zisizopatikana

?
Kampuni ya vyombo vya Habari
Halisia

Maelezo yote

Mwaka wa kuanzishwa

April 1994

Mwanzilishi

Dr. Reginald Mengi - ni mwanaviwanda wa Tanzania, mmiliki wa vyombo vya habari na muasisi, pia ni Mwenyekiti mtendaji wa IPP Group. Pia ni Makamu wa Rais wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania. Katika taarifa za FORBES, Mengi ni miongoni mwa mt

Mtendaji Mkuu

Beatrice Bandawe - Mhariri Mtendaji.

Mhariri Mkuu

Wallace Mauggo - mwandishi wa habari mkongwe. Alijiunga na Maelezo mwaka1973. Baada ya wadhifa huu alihamishiwa Tanzania School of Journalism. Baadaye alijiunga na IPP media.

Mawasiliano

The Guardian Ltd

P.O.Box 31042; Dar es salaam

Tel.: +255222700735/7

Fax: +255222700146

E-Mail: info@guardian.co.tz

www.ippmedia.com/sw/nipashe

Taarifa za kifedha

Taarifa ya Kifedha

Taarifa zisizopatikana

Faida za uendeshaji

Taarifa zisizopatikana

Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)

Taarifa zisizopatikana

Isa katika soko

Taarifa zisizopatikana

Maelezo ya ziada

Taarifa ya ziada

Kwa mujibu wa utafiti wa GeoPoll (Agost 30 – 1 Sep 2018), kuhusu hadira uliyodhaminiwa na MOM Tanzania. Magazeti yenye maslahi maalumu kama vile habari za michezo hayakujumuishwa kwenye uchambuzi wa umiliki.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Reporters without borders
  • Funded by
    BMZ