Radio One
Redio One ni miongoni mwa vituo vya redio vya FM vinavyofanyakazi chini ya IPP Media Limited. Redio One ilianza shughuli zake pamoja na ITV (kituo cha televisheni) mwaka 1994.
Radio One ni kituo cha redio cha saa 24 (free to air), pia ni kituo cha redio cha biashara chenye makao makuu yake Dar es salaam, Tanzania. Vipindi vya Redio One vinahusu masuala mbalimbali kuanzia habari, michezo, matukio (ya nchini na kimataifa), maisha ya watu, burudani na vinginevyo.
Kama ilivyoelezwa kwenye ripoti ya Tanzania Media Measurement ya GeoPoll, kwa takwimu za robo mwaka ya pili, 2018, Redio One ni ya tano kwa wasikilizaji yenye XX.XXX% miongoni mwa vituo vya redio 20 nchini Tanzania.
Wakati Redio One ilipoanza matangazo yake kwa majaribio tarehe 23 Februari 1994 na kuanza matangazo yake kwa ukamilifu tarehe 11 Julai, 1994, ilianza kujikusanyia umaarufu miongoni mwa vijana.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka IPP Media Limited, Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), TCRA na Vyanzo vingine kama ilivyooneshwa hapa chini kuwa Redio One inamilikiwa na Dkt Reginald Abraham Mengi na IPP Media Limited, inayoendesha vituo vya televisheni, kituo cha redio na magazeti.
Mengi alizaliwa Tanzania mwaka 1944. Yeye ni mfadhili wa Kitanzania, mwanaviwanda, mmiliki wa vyombo vya habari na mwasisi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Group. Mengi pia ni Makamu wa Rais wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu FORBES, amekuwa miongoni mwa matajiri wa Afrika mwenye zaidi ya $400 milioni kwa takwimu za mwaka 2015.
Isa za hadhira
Aina ya umiliki
binafsi
Maeneo yanayofikiwa
Taifa
Aina ya maudhui
Maudhui huru
Kampuni ya vyombo vya Habari
IPP Media Limited
Muundo wa umiliki
IPP Media ni mali ya IPP Group, kampuni binafsi inayomilikiwa na kikundi cha kampuni zilizoanzishwa na Dr. Reginald Abraham Mengi miaka ya 1960. Mmiliki hisa hawakuoneshwa TCRA,
Haki ya kuchagua
Taarifa zisizopatikana
Mmiliki Binafsi
Kundi / Mmiliki Binafsi
Agapitus Leons Nguma
alikuwa katibu wa kampuni na mwanahisa. Amefariki dunia 1 Mei 2018. Alikuwa pia Mkurugenzi wa the Guardian Ltd.na Bonite Bottlers Ltd. Kitaaluma ni Mwanasheria.
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
Date of registration: February 3rd 1994 Start: January 23rd 1994 on a trial basis, inauguration on June 11th 1994
Mwanzilishi
Dr. Reginald Mengi - ni mwanaviwanda wa Tanzania, mmiliki wa vyombo vya habari na muasisi, pia ni Mwenyekiti mtendaji wa IPP Group. Pia ni Makamu wa Rais wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania. Katika taarifa za FORBES, Mengi ni miongoni mwa mt
Mtendaji Mkuu
Joyce Mhavile - aliwahi kufanyakazi ya utangazaji katika redio na TV, IPP (ITV na Radio One). Baadae alipandishwa cheo kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu.
Mhariri Mkuu
Taarifa zisizopatikana
Mawasiliano
Radio One
P. O. Box 4374, DAR ES SALAAM
Tel: +255767777147
Fax: +255 22 2775915
E-Mail: itv@ipp.co.tz
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Isa katika soko
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Kiwango cha hadhira kwa mujibu wa ripoti ya viwango vya GeoPoll ya Redio & TV (Aprili – Juni 2018).
Muhtasari wa vyombo vya habari
Reginald Abraham Mengi (2018), I Can, I must, I will. ISBN-10: 9781717871749.