This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/03/19 at 10:16
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

The Citizen

THE CITIZEN, ni Gazeti la Kila Siku la Lugha ya Kiingereza lililosajiliwa kwa msajili wa Magazeti 7 Machi, 2014 na toleo la kwanza lilizinduliwa 16 Septemba 2014. Toleo lake la Jumapili linaitwa THE SUNDAY CITIZEN. Gazeti hili linatoa habari za uchambuzi za biashara na siasa na kuwalenga watoa uamuzi na wajasiriamali.

THE CITIZEN inakuwa na magazine/vijarida sita ndani yake vya mada tofauti kwa siku tofauti za wiki. Kila jumatatu gazeti hili linatoa kijarida cha “Your Health”, ni kijarida cha afya na cha mapitio ya siasa kijulikanacho kuwa “Political Forum”. Kila Ijumaa, huchapisha kijarida kijulikanacho kuwa ni “The Beat kuhusu burudani na showbiz” utumbuizaji watu, wakati kila Alhamisi, The Citizen huchapisha kijarida cha “Business Week”. Kijarida cha wanawake, “Woman” huchapishwa Jumamosi na “Sound Living” yaani maisha bora, ni kijarida cha mambo ya familia chenye kuchapisha makala za kujiongeza za matukio yaliyotokea katika jamii na kuchapishwa na kuandikwa na The Citizen.

THE CITIZEN linachapishwa na Mwananchi Communications Limited ambayo pia huchapisha gazeti la Kiswahili la MWANANCHI na toleo la jumpili la MWANANCHI JUMAPILI na MWANASPOTI, gazeti la michezo na burudani linalotoka mara mbili kwa wiki lililozinduliwa 12 Februari, 2001. Kampuni hii pia huchapisha vijarida kwa lugha ya kiswahili na vya kuchomoa kwa mada tofauti na kwa siku tofauti za wiki na kuchapishwa kwenye MWANANCHI.

Mwananchi Communications Limited was ilianzishwa mwaka 2001 na Balozi Ferdinand Ruhinda kwa ubia na Rostam Aziz. Kabla ya hapo, Balozi Ruhinda alikwisha anzisha kampuni ya mawasiliano ya Media Communications Limited imwaka 1999 ambapo mwaka 2001 ikawa Mwananchi Communication Company. Mwezi Desemba 2002, kampuni ya Kenya ya Nation Media Group ilinunua na kuwa na hisa nyingi ingawa hivi sasa ina hisa 41% tu hali ya kuwa Jehangir Kermali Bhaloo ana hisa 51%.

Taarifa muhimu

Isa za hadhira

Aina ya umiliki

binafsi

Maeneo yanayofikiwa

National (mainland)

Aina ya maudhui

maudhui yaliyolipiwa

Uwazi hafifu

Upatikanaji wa taarifa za wamiliki kutoka kwenye kampuni/chaneli

3 ♥

Kampuni ya vyombo vya Habari

Mwananchi Communications Limited

Nation Media Group Limited

Umiliki

Muundo wa umiliki

MCL inachapisha kama kampuni tanzu ya National Media Group inayoendeshwa na Aga Khan Foundation na kugharimiwa kupitia Aga Khan Development Fund. Mabadiliko ya umiliki ya hivi karibuni hayajaoneshwa BRELA ambako Aziz na Ruhinda wameoneshwa kama wanahisa. Wanahisa wa sasa kwa mujibu wa MAENDELEO (Juni 29, 2018).

Haki ya kuchagua

Taarifa zisizopatikana

Kundi / Mmiliki Binafsi

Jeangir Kermalzi Bhalov

Raia wa Tanzania

51%

Mmiliki Binafsi

Kampuni ya vyombo vya Habari
Halisia

Maelezo yote

Mwaka wa kuanzishwa

March 7, 2014

Mwanzilishi

Aziz Rostam - ni mwanasiasa, mfanyabiashara na miongoni mwa Watanzania tajiri sana. alijiuzulu nyadhifa zote za CCM mwaka 2011. Ruhinda Ferdinand – Alikuwa Balozi wa Jamhuri ya watu wa China. Ni mwanachama wa chama tawala-

Mtendaji Mkuu

Francis Majige Nanai - ana zaidi ya miaka 12 ya uongozi mwandamizi katika mauzo, masoko na usimamizi kwa jumla. Alijiunga na Mwananchi Communications Limited Ofisa Mwendeshaji Mkuu mwaka 2013 kabla ya kuteuliwa katika washifa wake wa sasa Agosti, 2014. J

Mhariri Mkuu

Bakari Machumu - Mhariri Mtendaji . Frank Sanga - Mkuu wa Ubunifu wa Maudhui. Damas Kanyabwinya - Mhariri.

Watu wengine muhimu

wa mujibu wa wasifu wa kampuni kutoka BRELA , wamekuwa wakurugenzi tangu Oktoba mwaka 2018:

Mawasiliano

Mwananchi Communications Limited (MCL)

P.O Box 19754, Dar es Salaam

Tel.: +255754780647

Fax: +255222224875

www.thecitizen.co.tz

Taarifa za kifedha

Taarifa ya Kifedha

Taarifa zisizopatikana

Faida za uendeshaji

Taarifa zisizopatikana

Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)

Taarifa zisizopatikana

Isa katika soko

Taarifa zisizopatikana

Maelezo ya ziada

Taarifa ya ziada

Kwa mujibu wa utafiti wa GeoPoll (Agost 30 – 1 Sep 2018), kuhusu hadira uliyodhaminiwa na MOM Tanzania. Magazeti yenye maslahi maalumu kama vile habari za michezo hayakujumuishwa kwenye uchambuzi wa umiliki.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ