Uhuru
Gazeti la UHURU ni gazeti la Kiswahili la kila siku linalochapishwa na UHURU Publications Limited kamopuni tanzu ya UHURU Media Group inayomilikiwa na Chama cha Mapunduzi, ambacho ni muungano baina ya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro Shirazi Party (ASD)
UHURU inajali zaidi hotuba za viongozi wa CCM na viongozi wa serikali, wengi wao ni makada wa Chama . Habari zake na zake na maoni ya mhariri zinasemekana kuandikwa kwa mtazamo wa CCM na serikali yake. Limetenga nafasi kuwaelimisha na kuwaarifu watu kuhusu utekelezaji wa Ilani ya CCM na masuala mengine muhimu ya kitaifa, kama vile sera za serikali. Dira ya 2025 ina programu nyingine za maendeleo.
Badaa ya kuanzishwa kwa Azimio la Arusha, waraka rasmi wa siasa ya ujamaa na kujitegemea 1, February, 1967. UHURU limetenga nafasi yake nyingi kusini , miongoni mwa mambo mwengine, itikadi ya ujamaa kama ilivyofafanuliwa kwenye Azimio la Arusha na kuanzisha mijadala kuhusu , mada zinazohusiana na maendeleo ya jamii ya kijamaa. Mhariri wa UHURU , Benjamini Mkapa baadaye amekuwa Rais wa Awamu ya Tatu wa Tanzania, alisema 1967 kuwa magazeti ya chama “wakati wote yanatakiwa kuielezea Serikali “ na “kuwaambia watu walioko kwenye nyadhifa muhimu waachane na mitazamo yao ya kikoloni”.
Historia ya UHURU imeanzia 1954 wakati TANU ilipoanzishwa na kuanzisha gazeti la SAUTI YA TANU, kuwainganisha watu wa Tanzania bora katika harakati zao za kizalendo na kitaifa na kitaifa ya kupata uhuru. Gazeti hili lilihaririwa na Rais wa TANU, Julius Kambarage Nyerere ambaye baada ya uhuru akawa Mwasisi, Rais wa Kwanza na Baba wa Taifa.
Siku ya uhuru, 9 Desemba 1961, gazeti la kihistoria la SAUTI YA TANU limebadilishwa na gazeti la wiki la UHURU ambalo chini ya jina la gazeti kulikuwa na jina dogo la GAZETI LA TANU . Lengo la UHURU ni “kuongoza njia ya uhuru na mshikamaono wa Tanganyika kwa ajili ya harakati za mapambano ya watu wote Duniani “. Katika maoni yake ya kwanza ya mhariri, gazeti hili lilithibitisha kwamba ni mali ya TANU wakati lilipoandika kuwa “Leo ni siku ya shangwe na Furaha, ni siku ya kuzaliwa gazeti la UHURU, gazeti la TANU”
Gazeti la UHURU limejiabainisha kuwa ni “gazeti la raia”na mwelimishaji”. Ni gazeti lenye jukumu la kujenga taifa jipya la Tanganyika. Ni gazeti la Taifa. UHURU ni gazeti lenu”.
Gazeti la UHURU ni la kisisa kwenye ripoti na maoni ya mhariri yake, na huitenga nafasi yake kubwa kwa mapambano ya kujikomboa ya nchi za Afrika zilizoko chini ya utawala na mamlaka ya kikoloni.
Na gazeti hili lina kiwango kikubwa cha kuwasili wananchi na mhariri wake Joel Mgogo amekiri kuwa ametenga 90% ya nafasi ya gazeti kuhubiri na kunasihi. Amenukuliwa kusema “kama sifanyi mimi atafanya nani?” Akitoa maoni ya tamko hilo John Condon amesema “Iwapo Rais Nyerere ni Mwalimu rasmi wa Taifa gazeti la chama ni mhubiri”Unasihi wote umetokana na uzingatiaji mkubwa uliopewa kwa hotuba za wanasiasa wa TANU na wale wa Serikali. Kwa hiyo UHURU halikuwa la kibiashara na wala halikukusudiwa kuwa hivyo, lipo kwa ajili ya kuipa TANU na Serikali yake mahali pa kutolea kauli zake ndani na nje ya nchi”.
Tarehe 7 Aprili , 1967, TANU ilianzisha gazeti la Kiingereza la kila wiki la The Nationalist lenye sera ya uhariri isiyotofautiana na ile ya UHURU wa kubadilishwa kuwa la kila siku, mwaka 1964. The Nationalist nalo baadaye lilibadilishwa kuwa la kila siku lakini liliunganishwa kuwa la kila siku lakini liliunganishwa na The Standard Tanzania 26 April 1972 kuwa Daily News baada ya utaifishaji wa standard – Tanzania 5 February 1970. TANU ilianzisha gazeti la MZALENDO tarehe 90 Aprili 1972 kama toleo la Jumapili la UHURU.
Isa za hadhira
Aina ya umiliki
Binafsi
Maeneo yanayofikiwa
National (mainland)
Aina ya maudhui
Maudhui yaliyolipiwa
Kampuni ya vyombo vya Habari
Uhuru Publications Limited
Muundo wa umiliki
Uhuru Publication Limited inamilikiwa na Chama tawala cha CCM. Taarifa za BRELA zimeombwa lakini hazikupatikana
Haki ya kuchagua
Taarifa zisizopatikana
Mmiliki Binafsi
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
Launched on independence day (December 9th 1961), the sucessor of Sauti ya TANU.
Mwanzilishi
Tanganyika African National Union (TANU) - kilikuwa chama kikuu cha siasa kilichogombea dola katika nchi ya Afrika Mashariki ya Tanganyika (ambayo sasa ni Tanzania). Chama cha TANU kilianzishwa kutoka Tanganyika African Association na Julius Nyerere mwe
Mtendaji Mkuu
Ernest Sungura - Kiongozi mkuu wa Uhuru Media Group. Alianzisha Tanzania Media Foundation (TMF) na alijiuzulu mwaka 2018, wakati akijiunga na chama.
Mhariri Mkuu
Kiondo Mshana - mwandishi wa habari anayefanya kazi na IPP media outlets. Ni mfawidhi wa Uhuru kama mhariri mtendaji
Mawasiliano
Taarifa zisizopatikana
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Isa katika soko
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Kwa mujibu wa utafiti wa GeoPoll (Agost 30 – 1 Sep 2018), kuhusu hadira uliyodhaminiwa na MOM Tanzania. Magazeti yenye maslahi maalumu kama vile habari za michezo hayakujumuishwa kwenye uchambuzi wa umiliki.
Muhtasari wa vyombo vya habari
John Condon (2013). Nation Building and Image Building in the Tanzania Press. Journal Of Modern African Studies, Vol 5, pp. 355 -354.
Hadji Konde (1984). Press Freedom in Tanzania. East African Publishing House.
Former Managing Editor, UHURU and MZALENDO (October 2018). Media Ownership Monitor Questionnaire UHURU.