This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/03/19 at 11:27
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Gazeti

Kanzi data ya Gazeti

Hadi Septemba 2018, magazeti 175 yalikuwa yamesajiliwa rasmi MAELEZO. Idadi hii ni ndogo sana ikilinganishwa na miaka miwili tu iliyopita wakati zaidi ya magazeti 400 yalikuwa sokoni. Kupungua kwa magazeti hakutokani tu na kupungua kwa mapato ya usambazaji au matangazo tu – kutokana na watangazaji kuanza kupitisha matangazo yao mitandaoni.

Pia inasababishwa na serikali kuzidi kuzibana kampuni za uchapishaji. Mwaka 2016, imefuta zaidi ya magazeti 400 na majarida, na kuyaambia yasajiliwe upya. Kufutwa kwa magazeti hayo kumepunguza idadi ya machapisho kwa zaidi ya 50%, na pia kuwa na athari za muda mrefu. Inaelekea kuwatishia wawekezaji wapya: mwaka 2016 magazeti 26 yalikuwa yamesajiliwa, yamepungua kutoka 39 yaliyosajiliwa mwaka 2015.

Kiwango kikubwa cha wingi wa wasomaji kinahatarisha wingi na aina za magazeti

MOM imeangalia kampuni 4 za juu kwa magazeti yanayolenga soko la habari. Mwananchi Communication Limited (MCL), chini ya Nation Media Group,IPP Media Group, New Habari (2006) Ltd, na Tanzania Standard Newspaper Ltd (TSN) linalomilikiwa na serikali. Kampuni hizo kwa pamoja kupitia magazeti yao ya habari huwafikia wasomaji XX.XXX%  MCL inamilikiwa binafsi na huendeshwa chini ya Nation Media Group iliyoko Kenya na kugharimiwa na The Aga Khan Development Fund.  IPP Media Group ni kampuni binafsi, inayomilikiwa na mfanyabiashara maarufu aliyefanikiwa, Dkt Reginald Mengi. New Habari (2006) Ltd, inahusishwa na mwanasiasa  na mfanyabiashara, Rostam Aziz, hali ya kuwa wanahisa hawafahamiki, isipokuwa baadhi ya tetesi zinaeleza kuhusiana na Aziz.

Serikali inamiliki magazeti mawili ya kila siku, wakati vyama vikuu viwili vya siasa vinahusishwa kila kimoja na gazeti moja la kila siku (CCM, UHURU, CHADEMA: Tanzania Daima). Hata hivyo, serikali imesajili magazeti 33, na mengi yao yanamilikiwa binafsi (116). Magazeti mengine yaliyobaki yanamilikiwa na taasisi za Dini.

Magazeti yamestahili panapofaa

Kwa mujibu wa Afrobarometer2017, ni asilimia 28 tu ya watu wanasoma magazeti angalau mara moja kwa mwezi. Asilimia 56 hawasomi kabisa magazeti. Watanzania wengi, hasa katika maeneo ya vijijini hawasomi kabisa magazeti. Kutokujua kusoma, kuandika na kuhesabu pamoja na masuala ya uwezo wa kununua, kumejenga mazingira magumu kwa magazeti. Watanzania wengi hasa wa vijijini wanaona kusoma magazeti ni anasa, badala yake wanapenda kusikiliza redio. Sababu nyingine inayohusiana na kushuka kwa mauzo ya magazeti ni tabia ya vituo vya redio na televisheni kupitia magazeti ya kila siku kwa kina badala ya kudokeza mambo muhimu tu kwa ufupi.

Kusema kweli magazeti yamefikia mahali pabaya; usambazaji magazeti kwenye maeneo mbalimbali nchini ni changamoto kubwa, usambazaji ulikuwa na bado uko kwenye baadhi ya mikoa muhimu tu.

Watanzania wanapenda kusoma kwa Kiswahili - na kuhusu michezo

Wakati wowote Watanzania wanaposoma, wanapenda kufanya hivyo kwa Kiswahili. Magazeti kwa lugha ya taifa yako ya aina mbalimbali kwa wasomaji kuchagua, kulinganisha na ya kiingereza yanayoonekana kuwalenga wasomi na wenye uwezo zaidi. Ni magazeti ya The Citizen na The Guardian tu ndiyo yapo kwenye magazeti 10 ya juu yanayochapisha pia habari za kijamii na kisiasa. 

Miongoni mwa magazeti 10 ya juu, ni ya idadi kubwa ya magazeti ya michezo – 5 kati ya 10 yanayopendwa zaidi yanatoa habari za michezo hasa mpira wa miguu na mpira wa kikapi, n.k.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ