This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/03/28 at 08:22
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Millard A. Ayo

Millard A. Ayo

Millard Afrael Ayo ni mwanzilishi wa Ayo Tv TZA Company Limited inayoendesha Millardayo.com. Alizaliwa 16 January, 1986, Arusha, Tanzania.

Uzoefu wa Ayo kwenye vyombo vya habari umeanza zamani alipokuwa na umri wa miaka 13, alichaguliwa kushiriki katika kipindi cha watoto kinachotangazwa na Clouds FM. Ilipofika mwaka 2005 alianza kufanyakazi na vyombo vya habari mbalimbali, miongoni mwao ni TVZ Zanzibar kama ripota wa habari kwa miezi 6. Halafu alijiunga na Wapo Radio, redio ya kikristo iliyopo Dar es salaam mwezi Mei 2005 alikofanyakazi kwa miaka mitatu bila ya mshahara.

Mwaka 2008, Millard Ayo alifanikiwa kujiunga na ITV na Radio One (IPP Media Limited) alikoendesha vipindi mbalimbali na kulipwa mshahara wa mwezi wa 300,000/=. Jina lake lilianza kukua na kujipatia umaarufu nchini Tanzania. Baada ya maombi yake ya kazi kukataliwa mara nyingi Clouds Fm, hatimaye alipata nafasi mwaka 2010 ambako anafanyakazi hadi sasa (2018).

Licha ya kumiliki chombo cha habari mtandaoni na blog, Millard Ayo anafanyakazi chombo cha habari kikubwa zaidi Tanzania (Clouds Media) kama mtangazaji wa Radio (Amplifier) na studio yake mwenyewe (“Ayo Studio”) hasa ikijishughulisha na utayarishaji wa habari, chama cha siasa cha Millard Ayo hakifahamiki kwa mujibu wa taarifa zake, hata hivyo anaungwa mkono na wanasiasa maarufu na watangazaji wa vyombo vya habari.

Ayo amepata tunzo km vile Best Presenter Radio Awards (2006), Best Website by Vodacom Tanzania na African Stars Family (Millardayo.com.2012). Mwaka alitangazwa na Africa Youth Awarda miongoni mwa Vijana wa kiafrica maarufu sana 100.

Millard alisoma shule ya msingi Patandi na shule ya Sekondari ya O’level, Akeni Secondary School zote za Arusha, baadaye alijiunga A’level Secondary School, Mbezi Beach Secondary, Dar es salaam alikohitimu mwaka 2002. Alijiunga na Arusha College of Electronics mwaka 2004, alijiunga na East Africa Training Institute, Arusha alikojifunza Uandishi wa Habari na Utangazaji. Ni motto wa kwanza katika familia ya watoto wane kwa wazazi wake Afrael Ayo (mfanya biashara mdogo mdogo) na Mary Ayo (Mwalimu).

Kampuni ya vyombo vya Habari
Aina za vyombo vya habari
  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ