This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-rsf.org/en/ retrieved on 2022/05/21 at 12:33
Reporters Without Borders (RSF) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Reporters without borders

Familia ya Bakhresa

Familia ya Bakhresa

Said Salimu Awadh Bakhresa ni mfanyabiashara mwenye mafanikio na uzoefu wa zaidi ya miaka 30 wa kusimamia kundi la kampuni za biashara. Yeye ni mwasisi na mwenyekiti wa Bakhresa Group of Companies. Alizaliwa mwaka 1949 na kukulia Zanzibar.

Bakhresa Group ni mkusanyiko wa kampuni mbalimbali zilizosajiliwa zinazofanya uchakataji wa mazao ya kilimo, vyakula na vinywaji baridi, usafiri wa majini, ufungashaji, usafirishaji, urejelezi wa plastiki na vyombo vya habari. Pia anaendesha hoteli huki Zanzibar inayoitwa Hotel Verde.

Mwanaviwanda maarufu anayefahamika Afrika Amshariki na Kati yote, Bakhresa aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuwa muuzaji wa urojo, kabla ya kujishughulisha kama mwendesha mkahawa katika miaka ya 1970. Kutokana na kuanza bila ya makuu aliunda himaya ya biashara ndani ya kipindi cha miongo mitatu tu. amemuoa Fathiya Bakhresa na wana watoto saba: Mohamed Said Salim Bakhresa, Abubakar Said Salim Bakhresa, Omar Said Salim Bakhresa , Yusuph Said Salim Bakhresa, Khalid Said Salim Bakhresa (amefariki 2007), Mariam Said Salim Bakhresa. Bakhresa Group ni biashara ya familia. Watoto wake wote ni Wakurugenzi Watendaji wa Salim bakhresa & Co Ltd yenye hisa nyingi katika Azam Media Limited. Watoto wake pia wana nyadhifa zifuatazo:

Yusuph Said Salim Bakhresa: Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Limited na Mkurugenzi wa Group Companies. Anashiriki kila siku kwenye shughuli za Bakhresa Food Products Ltd.

Abubakar Said Salim Bakhresa: Anasimamia Bakhresa Malawi Limited, Bakhresa Grain Milling (Rwanda), Bakhresa Grain Milling Limitada (Msumbiji) na Bakhresa South Africa (Pty) Limited. Ana shahada ya kwanza ya Sayansi katika Usimamizi wa Biashara, somo kuu likiwa Fedha kutoka Chuo kikuu cha George Town, Washington D.C USA. Anajihusisha zaidi na biashara za usindikaji ngano katika Group na anasimamia ununuzi wa ngano kwa ajili ya Group.

Mohamed Said Salim Bakhresa: Ni mkurugenzi Mtendaji wa Bakhresa Grain Milling (Uganda) Limited, kiwanda kikubwa zaidi cha kusindika ngano nchini Uganda. Amehitimu katika fedha,Sheria na utunzaji fedha kutoka chuo kikuu cha Southbank, United Kingdom.

Kampuni ya vyombo vya Habari
Aina za vyombo vya habari
Halisia

Biashara

Biashara zifuatazo zinaendeshwa chini ya kampuni mama:

Agro Commodities

Bakhresa Agro Commodities (PTY) Ltd – India

Food & Beverages

Azam Bakeries Co Ltd

Speciality Packaging

Omar Packaging Industries Ltd

Logistics

SSB Azam ICD Division

Petrolium

United Petroleum – (UP) is a market leader in the petroleum industry in Zanzibar

Transportation

Azam Marine Co Ltd & Kilimanjaro Fast Ferries Ltd

Agro Processing

Zanzibar Milling Cooperation Ltd.

Insurance

Azam Insurance Agency Ltd

Financial Services

AzamPay Tanzania Ltd

Corporate Social Responibility

Azam Football Club

Hospitality

Hotel Verde Zanzibar -Azam Luxy Resort & spa Ltd

Real Estate

Reliable Properties Ltd (Real Estate)

Manufacturing

Tradegents Ltd (Garments)

Familia & Marafiki

Maslahi jumuishi ya wanafamilia + Marafiki

Bakhresa Group is a family business.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Reporters without borders
  • Funded by
    BMZ