This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/04/18 at 15:33
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Azam Media Limited

Azam Media Limited

Azam Media Limited(AML) ni kampuni ya utangazaji kwa televisheni iliyosajiliwa Desemba, 2013. Ingawa ni mpya katika tasnia ya utangazaji, AML kwa kipindi cha miaka michache tangu ianzishwe, imekuwa miongoni mwa kampuni za vyombo vya habari vyenye miundombinu bora zaidi ya utangazaji. AML inayoendesha huduma ya TV ya kulipia inapatikana katika DHT.

AML ni kampuni tanzu ya Bakhresa Group, ni kampuni ya biashara inayomilikiwa na familia na miongoni mwa kampuni za viwanda zinazoongoza Tanzania yenye uwekezaji hasa katika sekta ya chakula na vinywaji baridi, ufungashaji, usafirishaji, huduma za usafiri majini, petrol na burudani. Kundi hilo la kampuni inajivunia moja ya timu kubwa za mpira Tanzania – Azam Football Club. Kwa mujibu wa tovuti yao, Bakhresa Group ina mapato ya zaidi ya USD milioni mia nane na zaidi ya watumishi elfu nane. Ilianzoshwa na Said Salim Awadh Bakhresa, ni mwanaviwanda maarufu aliyeanza kama mmiliki mdogo wa mkahawa miaka ya 1970 na kujenga himaya ya biashara ndani ya kipindi cha miongo mine. Saidi Salim Bakhresa bado ni mwenyekiti wa Bakhresa Group.

Azam Media Limited inasimamiwa na Yusuf Said Salim Bakhresa, miongoni mwa watoto wane wa mwasisi wa Bakhresa Group. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania – TCRA, Yusuf Said pia ni mwanahisa wa Azam Media Limited kama walivyo ndugu zake Abubakar Said Salim Bakhresa, Omar Said Salim Bakhresa na Mohamed Said Salim Bakhresa. Kila mmoja anamiliki 5% ya hisa, wakati Said Salim Bakhresa & Co Ltd – ambayo pia ni kampuni tanzu ya Bakhresa Group of Companies anamiliki 80% ya hisa zilizobaki.

Ndugu hao wote wapo kwenye bodi ya wakurugenzi ya Bakhresa Group, yenye shughuli zake Afrika Mashariki yote, Malawi, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Afrika Kusini.

Azam Media is imesajiliwa, Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) (N0.95870) na jalada la kampuni lilipatikana. Limeorodhesha wanahisa waliotajwa hapo juu, pia imetaja rehani tarehe 12 Juni, 2013 kwa Standard Chartered Bank Tanzania Limited kupata USD 8,000,000. Mapato ya kila mwaka yameripotiwa hadi 2017.

Taarifa muhimu

Kampuni Mama

Bakhresa Group of Companies

Aina ya Biashara

Binafsi

Mfumo kisheria

Kampuni ya dhima yenye kikomo

Nyanja za Kibiashara

Azam Media Limited - Utangazaji. Bakresha Group of Companies - uwekezaji zaidi kwenye sekta vyakula na vinywaji, ufungashaji, usafirishaji, Usafirishaji abiria baharini, bidhaa za petroli na burudani.

Umiliki

Mmiliki Binafsi

Familia ya Bakhresa

Said Salim Bakhresa & Co. Ltd - ni kampuni kubwa ya Bakhresa Group. Ilianzishwa mwaka 1983, jijini Dar Es Salaam, Tanzania, SSB ina kiwanda kikubwa cha usaji wa ngano na maghala ya uhifadhi makubwa Afrika Mashariki naajira ya moja kwa moja ya watu 1000

80%
Vyombo vya habari
Other Media Outlets

Televisheni zingine

Azam One

Digitali nyingine

registered as a Online Content Service at TCRA.

Halisia

Chombo cha habari cha kibiashara

Broadcast

Azam FM Radio Ltd

Online Content Services

Azam Media Limited

Biashara

Business activities of Bakhresa Group of Companies are regional, especially Tanzania Mainland & Zanzibar, Kenya, Uganda, Malawi, Mozambique, Zambia, Rwanda, Burundi and in South Africa.

Following businesses are operated uneder the umbrella of the mother company:

Agro Commodities

Bakhresa Agro Commodities (PTY) Ltd – India

Food & Beverages

Azam Bakeries Co Ltd

Speciality Packaging

Omar Packaging Industries Ltd

Logistics

SSB Azam ICD Division

Petrolium

United Petroleum – (UP) is a market leader in the petroleum industry in Zanzibar

Transportation

Azam Marine Co Ltd & Kilimanjaro Fast Ferries Ltd

Agro Processing

Zanzibar Milling Cooperation Ltd.

Insurance

Azam Insurance Agency Ltd

Financial Services

AzamPay Tanzania Ltd

Corporate Social Responibility

Azam Football Club

Hospitality

Hotel Verde Zanzibar -Azam Luxy Resort & spa Ltd

Real Estate

Reliable Properties Ltd (Real Estate)

Manufacturing

Tradegents Ltd (Garments)

Maelezo yote

Mwaka wa kuanzishwa

14th December, 2012

Mwanzilishi

Said Salim Awadh Bakhresa - is a successful businessman with over 30 years’ experience of managing a group of complex businesses. He is the founder and chairperson of Bakhresa Group of Companies.

Waajiriwa

Azam Media Limited: no information. Bakresha Group: more than 8000.

Mawasiliano

Plot No. 46/4, Nyerere Road, Ilala, Dar es Salaam.

Namba ya kutambulika

BRELA incorporation n°95870

Taarifa za kifedha

Taarifa ya Kifedha

Taarifa zisizopatikana

Faida za uendeshaji

Taarifa zisizopatikana

Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)

Taarifa zisizopatikana

Utawala

Bodi ya utendaji + Bodi Maslahi ya utendaji

Said Salim Awadh Bakhresa

Chairman, Bakhresa Group of Companies. He is the founding father and the Chairman of the Bakhresa Group of Companies. He is a well-known industrialist in the region.

Bodi isiyo ya utendaji + Bodi maslahi isiyo ya utendaji

Taarifa zisizopatikana

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ