This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/03/28 at 20:29
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Uhuru Publications Limited

UHURU Publications Limited (UPL) ni miongoni mwa wachapishaji wakubwa nchini Tanzania. Ilianzishwa na Chama cha Mapinduzi mwanzoni mwa mwaka 1990. Kampuni hii inachapisha gazeti la kila siku la UHURU na magazeti mengine mawili ya kila wiki ya MZALENDU na BURDANI ambalo ni la kujiburudisha.

Historia ya UHURU Publications Limited inaanzia Aprili 1962 wakati Tanganyika African National Union (TANU) ilipoanzisha Mwananchi Printing and Publishing Company ambayo Bodi ya Wakurugenzi wake ilijazwa na Mawaziri, wanasiasa na makada wa chama. Mwaka 1966, baada ya mapendekezo ya serikali, TANU ilikubali kuigawa Mwananchi Printing and Publishing Company kuwa kampuni mbili. Uchapishaji ulikuwa kwenye kampuni mpya iliyoundwa ya National Printing Company (Kiwanda cha Taifa cha Uchapaji –KIUT) iliyokuwa chini ya National Development Corporation (NDC) wakati uchapishaji ulibakia kwenye kampuni iliyoundwa mpya ya Mwananchi Publishing Company (1966) Limited. Hata hivyo, Mwananchi Publishing Company (1966) Ltd ilibadilishwa jina na kuwa Shirika la Magazeti ya Chama ambalo mwanzoni mwa miaka ya 1990 lilibadilishwa tena na kuitwa UHURU Publications Limited. UPL ilinunua mashine ya uchapaji ya web-offset mwaka 1995 na kuiendesha chini ya kampuni tanzu ya Modern Newspapers Printers, na kuifanya UHURU kuwa gazeti la kwanza la Kiswahili la nchini kuchapishwa kwa rangi kwenye mitambo yake.

Kutokana na makubaliano yaliyotokea mwaka 1966, Benjamin William Mkapa, aliyekuwa mhariri mtendaji wa TANU, iliyomiliki gaziti la The Nationalist baadaye alikuwa Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akawa mhariri mtendaji wa magazeti ya chama. Mhariri Mtendaji wa kwanza alikuwa Ronald Mwanjisi na kufuatiwa na Joel Mgogo.

Mhariri Mtendaji anateuliwa na Kamati Kuu ya CCM baada ya kupendekezwa na Bodi ya UPL. Kwa sasa UPL haina bodi baada ya wajumbe wao kujiuzulu Septemba 2016 baada ya ziara ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli, baada ya UPL na watumishi kumweleza kuhusu ubadhirifu na uongozi mbaya uliyopo UPL.

Taarifa muhimu

Kampuni Mama

UHURU Media Group

Aina ya Biashara

Binafsi

Mfumo kisheria

Kampuni ya dhima yenye kikomo

Nyanja za Kibiashara

Uhuru Publications Limited imesajiliwa (MAELEZO) Idara ya Habari Tanzania – Wizara ya Habari kama mchapishaji wa aina mbalimbali za magazeti

Umiliki

Mmiliki Binafsi

Chama Cha Mapinduzi (CCM)

ni muungano wa Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP), vyama viwili vya siasa vilivyoongoza harakati za uhuru Tanzania bara na Zanzibar mtawalia. Vyama hivyo viliungana 5 Februari, 1977.

?
Vyombo vya habari
Other Media Outlets

Magazeti mengine

Uhuru

Radio nyingine

Uhuru Radio

Halisia

Chombo cha habari cha kibiashara

Uhuru Publications Limited

Free Media Limited

Redio

People’s Communication Media

Biashara

hakuna

none

Maelezo yote

Mwaka wa kuanzishwa

Launched on independence day (December 9th 1961), the sucessor of Sauti ya TANU.

Mwanzilishi

Tanganyika African National Union (TANU) - was the principal political party in the struggle for sovereignty in the East African state of Tanganyika (now Tanzania). The party was formed from the Tanganyika African Association by Julius Nyerere in July 1954. From 1964 the party was called Tanzania African National Union.

Waajiriwa

Taarifa zisizopatikana

Mawasiliano

Uhuru Publications Limited

P. O. Box 9221

Dar Es Salaam

uhurunews@yahoo.com

tel: +255222183782

Fax: +255283780

Namba ya kutambulika

BRELA Incorporation N°62262

Taarifa za kifedha

Taarifa ya Kifedha

Taarifa zisizopatikana

Faida za uendeshaji

Taarifa zisizopatikana

Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)

Taarifa zisizopatikana

Utawala

Bodi ya utendaji + Bodi Maslahi ya utendaji

Currently, UPL has no Board after its members resigned in September 2016 following the visit of CCM Chairman and President of the United Republic of Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli, to UPL and employees told him about mismanagement and maladministration prevailing in UPL

Watu muhimu wenye ushawishi + watu maslahi wengine muhimu

Ernest Sungura (CEO) - Chief Leader Uhuru Media Group. He founded Tanzania Media Foundation (TMF) and has resigned in 2018, when he joined the party.

Maelezo ya ziada

Taarifa zisizopatikana

Taarifa za wamiliki wa vyombo vya Habari ambazo hazikupatikana, kampuni zakataa kutoa maelezo au hazikujibu au hazina hifadhi ya kumbukumbu zake

1 ♥

Taarifa ya ziada

Company registered at BRELA, profile requested, still pending. Questionnaires were not returned.

Vyanzo

Former Managing Editing, UHURU Publications Limited. Media Ownership Monitor Questionnaire UHURU Publications Limited.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ