Azam Two
Azam TV ni mtoa huduma binafsi kwa njia ya dijiti kupitia Satelaiti iliyopo Dar es salaam na kumilikiwa na Azam Media Limited, kampuni tanzu ya Bakhresa Group Companies. Azam TV imeanzishwa mwaka 2013, na kuwa miongoni vya vituo vya TV vyenye hadhira kubwa. Ni ya tatu nchini kwa kuwa na watazamaji wengi, XX.XXX% kwa mujibu wa utafiti war obo ya pili ya mwaka 2018, utafiti wa GeoPoll.
Ina vipindi vingi vikiwemo filamu, vipindi vya uhalisia, filamu za burudani ndefu, vipindi vya elimu, michezo na habari na matukio. Kituo hiki kinajivunia cheneli tatu zinazokidhi mahitaji ya aina zote za hadhira na hivyo kuwa miongoni mwa TV zinazopendwa kuangaliwa sana na makundi yote ya jamii.
Chaneli hizo ni: Azam One, inayoshughulikia vipindi vya makala kama vile Semina za Kiafrika, mechi za mpira na burudani kwa watoto; Azam Two, ni chaneli ya burudani ya kimataifa ambapo watazamaji watapata tamthilia, makala, mziki, sinema za mapenzi na Sinema Zetu inayotoa sinema mbalimbali a Bongo.
Azam Media Limited inasimamiwa na Yusuf Said Salim Bakhresa, miongoni mwa watoto wane wa mwasisi wa Bakhresa Group. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania–TCRA, Yusuf Said pia ni mwanahisa wa Azam Media Limited kama walivyo ndugu zake Abubakar Said Salim Bakhresa, Omar Said Salim Bakhresa na Mohamed Said Salim Bakhresa. Kila mmoja anamiliki 5% ya hisa, wakati Said Salim Bakhresa & Co Ltd – ambayo pia ni kampuni tanzu ya Bakhresa Group of Companies anamiliki 80% ya hisa zilizobaki.
Azam Media is imesajiliwa, Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) (N0.95870) na jalada la kampuni lilipatikana. Limeorodhesha wanahisa waliotajwa hapo juu, pia imetaja rehani tarehe 12 Juni, 2013 kwa Standard Chartered Bank Tanzania Limited kupata USD 8,000,000. Mapato ya kila mwaka yameripotiwa hadi 2017.
Isa za hadhira
Aina ya umiliki
Binafsi
Maeneo yanayofikiwa
Taifa
Aina ya maudhui
Free to Air
Kampuni ya vyombo vya Habari
Azam Media Limited
Muundo wa umiliki
Azam Two inaendeshwa na Azam Media Limited inayomilikiwa na kampuni ya familia ya Bakhresa Group.
Haki ya kuchagua
Taarifa zisizopatikana
Mmiliki Binafsi
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
2013
Mwanzilishi
Said Salim Awadh Bakhresa - ni mfanyabiashara mwenye mafanikio na uzoefu wa zaidi ya miaka 30 ya kusimamia kampuni yenye biashara mbalimbali. Ni muasisi na Mwenyekiti wa Bakhresa Group of Companies.
Mtendaji Mkuu
Yusuf Said Salim Bakhresa - ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Limited na pia ni Mkurugenzi wa the Group Companies. Anashiriki kwa ukamilifu katika shughuli za kila siku za Bakhresa food products Ltd. Yeye ni mtoto wa Said Salim.
Mhariri Mkuu
Tido Mhando - ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji. Aliwahi kufanyakazi na BBC Swahili Service mapema miaka ya 2000 kabya ya kujiunga na TBC kama Mtendaji Mkuu.. Kabla ya kujiunga na BBC, alifanyakazi Voice of Kenya (VoK) iliyopo Nairobi na Radio Tanzania Dar e
Mawasiliano
Azam Media Limited
P.O. Box: 2517, Dar-Es-Salaam
Tel.: +255687030580
E-Mail: hassan.mhelela@azam-media.com
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Isa katika soko
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Kiwango cha hadhira kwa mujibu wa ripoti ya viwango vya GeoPoll ya Redio & TV (Aprili – Juni 2018).