This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/03/28 at 10:41
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

ITV

Independent Television Limited ni kampuni tanzu/shiriki IPP Limited. ITV ilianza shughuli zake mwaka 1994 ikiwa na kituo kimoja cha televisheni na kimoja cha redio kinachojulikana kuwa ITV (Independent Television Limited) na Radio One, mtawalia.

ITV ni Free to Air Chanel nchini Tanzania bara, pia ni kituo cha TV cha biashara kinachotangaza kupitia masafa bora (VHF). Ripoti ya GeoPoll’s Tanzania Media Measurement yenye takwimu za hadhiri za robo mwaka ya pili ya 2018 zinazopimia utazamaji wa Vituo vya TV vinavyotazamwa sana na vituo vya radio vinavyosikilizwa sana nchini, imeiweka kituo cha ITV kuwa na hisa ya hadhira ya XX.XXX% na kuwa namba moja miongoni mwa vituo vya TV vyote nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa kampuni yenyewe, taarifa ya bahari ya saa 2:00 usiku (20:00 HRS) ndiyo inayoongoza kwa kuwa na watazamaji takribani 70% siku yoyote ile. Taarifa ya habari hutangaza habari za nchini, za kimataifa, za biashara na za michezo pia ITV inatangaza habari za nchini saa 12:00 asubuhi (06:00 HES) kuanzia Jumatatu hadi Jumapili na saa 5:00 usiku (23:00 HRS) Jumatatu mpaka Ijumaa. Licha ya hivyo, kituo hicho kinatangaza habari za saa kwa dakika tano kuanzia saa 2:55 asubuhi (08:55 HRS) mpaka saa 9:55 asubuhi na matangazo yake kusikika barani Afrika sehemu za mashariki ya kati na Ulaya. Zaidi ya 60% ya vipindi vyake ni vya nchini vinavyolenga familia yote na kujuisha umri wote na hali ya uchumi jamii.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Reginald Abraham Mengi na IPP Group Limited ni wamiliki wa Independent Television Limited (ITV). Mengi pia ni mtendaji Mkuu.

IPP Group Limited ni kampuni ya utengenezaji utiaji vinywaji kwenye chupa na kundi la vyombo vya habari inayojumuisha vituo vya televisheni na vya redio na magazeti. Wasifu wa kampuni uliyoombwa kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Utoaji wa Leseni (BRELA) unaonyesha kuwa Dkt Reginald Abraham Mengi na Agaptus Leon Nguma ni wanahisa wa IPP Group Limited.

Mengi alizaliwa Tanzania mwaka 1944, yeye ni mfadhili wa Kitanzania, mwana viwanda, mmiliki wa vyombo vya habari na mwasisi na mwenyekiti Mtendaji wa IPP Group. Mengi pia ni Makamu wa Rais wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) Tanzania . Katika taarifa ya FORBES, amekuwa ni miongoni mwa matajiri wa Afrika mwenye zaidi ya $400 Millioni kwa takwimu za 2015.

Taarifa muhimu

Isa za hadhira

Aina ya umiliki

Binafsi

Maeneo yanayofikiwa

Taifa

Aina ya maudhui

Free to Air

Taarifa zinazopatikana kiurahisi

Upatikanaji wa taarifa za umiliki kutoka kwa vyanzo vingine, kwa mfano vile vinavyotambulikana kisheria

2 ♥

Kampuni ya vyombo vya Habari

IPP Media Limited

Umiliki

Muundo wa umiliki

IPP Media ni mali ya IPP Group, kampuni binafsi inayomilikiwa na kikundi cha kampuni zilizoanzishwa na Dr. Reginald Abraham Mengi miaka ya 1960. Mmiliki hisa hawakuoneshwa TCRA, Julai 2018.

Haki ya kuchagua

Taarifa zisizopatikana

Mmiliki Binafsi

Kampuni ya vyombo vya Habari
Halisia

Maelezo yote

Mwaka wa kuanzishwa

Date of registration: January 17th 1994 Start: June 10th 1994

Mwanzilishi

Dr. Reginald Mengi - ni mwanaviwanda wa Tanzania, mmiliki wa vyombo vya habari na muasisi, pia ni Mwenyekiti mtendaji wa IPP Group. Pia ni Makamu wa Rais wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania. Katika taarifa za FORBES, Mengi ni miongoni mwa mt

Mtendaji Mkuu

Joyce Mhavile - aliwahi kufanyakazi ya utangazaji katika redio na TV, IPP (ITV na Radio One). Baadae alipandishwa cheo kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu

Mhariri Mkuu

Taarifa zisizopatikana

Mawasiliano

Independent Television (ITV)

P.O. Box 4374, Dar-Es-Salaam

Tel.: +255222775915/6

Fax: +255222775915

E-Mail: itv@ipp.co.tz

www.ippmedia.com

Taarifa za kifedha

Taarifa ya Kifedha

Taarifa zisizopatikana

Faida za uendeshaji

Taarifa zisizopatikana

Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)

Taarifa zisizopatikana

Isa katika soko

Taarifa zisizopatikana

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ