This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/03/28 at 21:35
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Radio Free Africa

Redio Free Africa ilianzishwa mwaka 1995 chini ya kifupisho maarufu cha RFA. Redio hii iliyopo Mwanza kwenye ziwa Victoria inatangaza kwa Kiswahili habari za kitaifa na kimataifa, burudani,, makala, matukio, maigizo, michezo na sitcoms.

Ni miongoni mwa vituo vya redio vinavyosikilizwa sana. Imekuwa kituo cha pili maarufu XX.XXX% kwa mujibu wa utafiti wa robo ya pili kuhusu hadhira ya wasikilizaji wa vituo vya redio nchini GeoPoll kwa mwaka 2018. Kituo hiki kinatangaza katika masafa 20 nchini kote. Vipindi vyake hufikia pia kanda ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini kupitia masafa ya FM na AM.

Baada ya kituo kuanza kutangaza kwa majaribio mwezi Agosti 1995, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) lilisita kuipa leseni ya kisheria. Kabla ya hapo, mwenyekiti Mtendaji Dkt. Anthony M. Diallo, alibaini kuwa, kimsingi, usajili ulikuwa mgumu kwa sababu tulilazimika kufuata taratibu zote za Serikali, kwa kuzingatia kuwa hata utawala wa Serikali haukuwa na uzoefu katika kipengele hiki “(barua kutoka kwa Anthony M. Diallo, Septemba 25, 1996)”.

Hivi sasa leseni ya redio ya RFA imesajiliwa kwenye Sahara Media Group Ltd (SMG) kwa 100% kwa mujibu wa Mamlaka ya MawasilianoTanzania (TCRA). SMG iliyokuwa ikiitwa Sahara Communication and Publishing Company Ltd, ilianzishwa mwaka 1992. Inaendesha vyombo vitatu vya habari vya Star TV, Redio Free Africa na Kiss FM.

Data za umiliki wa SMG hazikuweza kupatikana katika Wakala ya Usajili wa Biashara na Utoaji wa Leseni (BRELA). Kwa mujibu wa wasifu uliyounganishwa kwenye mtandao, Mwenyekiti na mtendaji mkuu wa SMG hadi sasa ni mwasisi wake Dkt. Anthony M. Diallo, alikuwa waziri katika nyadhifa mbalimbali.

Taarifa muhimu

Isa za hadhira

Aina ya umiliki

binafsi

Maeneo yanayofikiwa

Taifa (husikika ukanda wote wa mashariki, kati na kusini kupitia masafa ya FM na AM)

Aina ya maudhui

Maudhui huru

Taarifa zisizopatikana

Taarifa za wamiliki wa vyombo vya Habari ambazo hazikupatikana, kampuni zakataa kutoa maelezo au hazikujibu au hazina hifadhi ya kumbukumbu zake

1 ♥

Kampuni ya vyombo vya Habari

Sahara Media Group Limited

Umiliki

Muundo wa umiliki

Radio Free Africainamilikiwa na kuendeshwa na Sahara Media Group Limited,ambayo hatimaye inamilikiwa na mwasisi wake Dr. Diallo. Hakuna data zilizopatikana BRELA

Haki ya kuchagua

Taarifa zisizopatikana

Kampuni ya vyombo vya Habari
Halisia

Maelezo yote

Mwaka wa kuanzishwa

Date of registration: September 6th 1995 Start: August 1995 on a trial basis

Mwanzilishi

Dr. Anthony M. Diallo - ni mwanasiasa na mwenyekiti wa chama wa mkoa wa Mwanza wa chama tawala cha Chama cha Mapinduzi (CCM). Alikuwa mbunge (1995 - Okt 2010) na kupoteza ubunge kwa mgombea wa upinzani. Alikuwa na nyadhifa mbalimbali katika baraza la Mawa

Mtendaji Mkuu

Anthony M. Diallo - angalia hapo juu

Mhariri Mkuu

Beatrice Rabachi - Meneja wa Vipindi. Calvin Jilala - Mhariri wa Habari.

Mawasiliano

Radio Free Africa;

Plot No. 5-7, Ilemela Industrial Area, Airport Road,

P.O Box 1732, Mwanza.

E-mail: info@radiofreeafrica.co.tz

www.radiofreeafrica.co.tz

Taarifa za kifedha

Taarifa ya Kifedha

Taarifa zisizopatikana

Faida za uendeshaji

Taarifa zisizopatikana

Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)

Taarifa zisizopatikana

Isa katika soko

Taarifa zisizopatikana

Maelezo ya ziada

Taarifa ya ziada

Kiwango cha hadhira kwa mujibu wa ripoti ya viwango vya GeoPoll ya Redio & TV (Aprili – Juni 2018).

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ