Radio Maria
Radio Maria Tanzania ni kituo cha redio, kinachotangaza kutoka Dar es salaam kama sehemu ya mtandao wa vituo vya Redio vya Milan, Italy. Muundo wa vipindi vya Redio Maria Tanzania una makundi manne kama vile maarifa ya kiroho ya Watakatifu, habari na taarifa, uhamasishaji na ustawi wa mwanadamu, na mwisho ni jamii na burudani. Mara nyingi hupiga muziki wa Kikatoloki, Kikristo na Injili.
Kwa mujibu wa Ng’atigwa (2013),Radio Maria Tanzania (inayojulikana kwa RMT) na wito wa “Sauti ya Kikristo Nyumbani Kwako” nin kituo cha Redio cha FM kilichoanziswa mwaka 1996 manispaa ya Songea, kusini ya Tanzania. Kuanzishwa kwa RMT ni juhudi zilizofanywa na Archbishop Norbert Mtega, Jimbo la Askofu Mkuu wa Katoliki la Songea wakati wa mkutano wake na Rais wa Association of the World Family of Radio Maria, Italy, Uganda mwaka 1996. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), RTM inamilikiwa na World Family Radio Maria Africa kwa 51% na Fondazione Formore kwa 48% zilizobaki.
RMT inamilikiwa na kusimamiwa na The Association of Radio Maria Tanzania Company Limited. Wanachama wa The Association of Radio Maria Tanzania ni pamoja na “watu waliooa, kuolewa na wasioolewa na kuoa, maburuda na watawa, na makasisi na mapadre, hata hivyo, redio hii haimilikiwi na jimbo la askofu la katoliki lolote mahususi nchini Tanzania au mkutano na Maaskofu Tanzania.
Kutokana na matatizo ya vifaa, mahitaji ya uendeshaji huko Songea, RMT imehamishia studio yake kuu eneo la Mikocheni, jijini Dar es salaam mwaka 2003. Kituo kilisajiliwa na TCRA katika kundi la leseni isiyo ya kibiashara, kuendesha kama kituo cha redio cha dini na kuweka kipaumbele cha maudhui na malengo ya dini. Kama sharti la kundi hili la leseni, matangazo ya biashara ni marufuku.
Kwa mujibu wa hadhira/wasikilizaji katika utafiti wa GeoPoll (2018), Radio Maria ni ya 10 yenye XX.XXX% ya wasikilizaji miongoni mwa vituo 20 nchini Tanzania, na katika kanda ya kati kuna XX.XXX% ikilinganishwa na vituo vya redio vya dini vingine nchini.
HAdi Julai, 2011, RMT imefikia majimbo ya Askofu 13 kati ya Majimbo 33 ya Askofu ya Katoliki nchini Tanzania. Hata hivyo, kupitia matangazo yake kwa satelaiti yaliyoongezwa nguvu na transmita nane zilizopo kwenye maeneo tofauti ya Tanzania, matangazo ya kituo cha redio yanasikika takribani Tanzania nzima. RMT pia hupatikana kwenye mtandao kwa www.radiomaria.co.tz na kuweza kupatikana kwa kutumia ujumbe kwenye akaunti ya facebook.
Isa za hadhira
Aina ya umiliki
Binafsi isiyo ya biashara
Maeneo yanayofikiwa
Mkoani
Aina ya maudhui
Maudhui huru
Kampuni ya vyombo vya Habari
World Family of Radio Maria Africa
Muundo wa umiliki
Radio Maria inaendeshwa na World Family of Radio Maria Africa ambayo ni mali ya World Family of Radio Maria.
Haki ya kuchagua
Taarifa zisizopatikana
Kampuni
Kundi / Mmiliki Binafsi
Fondazione Formare
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
Date of registration: May 3rd 1996 Start: April 26th 1996
Mwanzilishi
Askofu Norbert Mtega / Jimbo la Askofu Mkuu wa Katoliki la Songea .
Mtendaji Mkuu
Taarifa zisizopatikana
Mhariri Mkuu
Taarifa zisizopatikana
Mawasiliano
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Isa katika soko
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Kiwango cha hadhira kwa mujibu wa ripoti ya viwango vya GeoPoll ya Redio & TV (Aprili – Juni 2018).