Tanzania Daima
Tanzania Daima ni Gazeti la Kiswahili la Kila Siku linalochapishwa na Free Media Limited. Gazeti hili linaandika masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa nchini Tanzania. Habari zake zinasemekana kukosoa chama tawala. Kwa mujibu wa utafiti wa GeoPoll kuhusu usomaji wa magazeti, uliyodhaminiwa na MCT (Aug/Sep 2018), Tanzania Daima ni miongoni mwa magazeti 10 ya juu lenye maudhui ya kijamii na kisiasa (XX.XXX% ya wasomaji).
Kwa maandishi, katika Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Dr. Lillian Mtei ametajwa kama mwasisi, mmiliki wa hisa nyingi (75%) na Mkurugenzi. Ameolewa na Freeman Mbowe ambaye ni mwanasiasa wa Tanzania na Mwenyekiti wa siasa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA –). Amechaguliwa kuendelea kuwa mbunge anayewakilisha Wilaya ya Hai katika Mkoa wa Kilimanjaro katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hivi sasa anaendelea na siasa kwenye chama hicho hicho cha siasa.
Nafasi ya Mbowe bado haifahamiki kwa sababu wasifu wa Kampuni katika Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni haukuweza kupatikana na kampuni haikujibu mahojiano kwa njia ya madodoso.
Isa za hadhira
Aina ya umiliki
Binafsi
Maeneo yanayofikiwa
taifa bara)
Aina ya maudhui
maudhui yaliyolipiwa
Kampuni ya vyombo vya Habari
Free Media Limited
Muundo wa umiliki
Tanzania Daima inaendeshwa na Free Media Limited, inayohusishwa na kiongozi wa chama cha upinzani, Freeman Mbowe. Mke wake anamiliki hisa nyingi
Haki ya kuchagua
Taarifa zisizopatikana
Kundi / Mmiliki Binafsi
Dr. Lilian Mtei
ni daktari wa tiba. Ni mke wa Freeman Mbowe, ambaye ni kiongozi mashuhuri wa chama cha siasa cha upinzani na Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anatoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Dudley Alphayo
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
registered at BRELA May 2004.
Mwanzilishi
Dr. Lilian Mtei - ni daktari wa tiba. Ni mke wa kiongozi maarufu wa upinzani Freeman Mbowe. Dudley Alphayo - ni anahisa chache na hasijulikani sana.
Mtendaji Mkuu
Taarifa zisizopatikana
Mhariri Mkuu
Martin Malera - Kaimu Mhariri Mtendaji. Tamali Vullu - Mhariri wa Habari.
Mawasiliano
Free Media
PO 15261, Dar es salaam.
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Isa katika soko
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Kwa mujibu wa utafiti wa GeoPoll (Agost 30 – 1 Sep 2018), kuhusu hadira uliyodhaminiwa na MOM Tanzania. Magazeti yenye maslahi maalumu kama vile habari za michezo hayakujumuishwa kwenye uchambuzi wa umiliki.