TBC FM
Chaneli hii ya redio imewalenga vijana. Kwa mujibu wa mahojiano na Director of Radio Services, TBC FM ni chaneli ya vijana, inayotangazwa na vijana na kwa ajili ya vijana. Watayarishaji ni vijana, maudhui yake yamekusudiwa kuhudumia maslahi ya vijana na walengwa wakuu ni hadhira ya vijana. Hata hivyo maadili ya utangazaji ni lazima yazingatiwe.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Tanzania Media Measurement ya GeoPoll, kwa takwimu za hadhira za robo mwaka ya pili ya 2018, TBC FM ina hadhira ya asilimia XX.XXX%. Kwa hiyo ni ya saba miongoni mwa vituo vya redio vyote.
Inamilikiwa na Tanzania Broadcasring Corporation ambayo ni chombo cha umma cha utangazaji pekee Tanzania Bara. Ni shirika la umma lililoanzishwa mwaka 1992 kwa mujibu wa Sheria ya Mashirika ya Umma, kutoa huduma ya utangazaji ya umma kwa njia ya redio na televisheni. TBC inamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Tanzania, na kusimamiwa na Msajili wa Hazina, idara ndani ya Wizara ya Fedha, yenye 100% ya hisa. Lengo la Serikali ni kutumia TBC kuongeza nguvu juhudi za serikali katika kujenga Taifa. Hatimaye, serikali inaitegemea TBC kuwa msemaji wake kuliko kutangaza kwa uhuru wake bila ya upendeleo.
Isa za hadhira
Aina ya umiliki
umma
Maeneo yanayofikiwa
Taifa
Aina ya maudhui
Maudhui huru
Kampuni ya vyombo vya Habari
Tanzanian Broadcasting Corporation
Muundo wa umiliki
TBC Taifa inaendeshwa kinadharia na umma lakini kwa vitendo inaendeshwa na Tanzanian Broadcasing Corporation inayomilikiwa na serikali
Haki ya kuchagua
Taarifa zisizopatikana
Mmiliki Binafsi
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
Started as„Sauti ya Dar es Salaam” (The Voice of Dar es Salaam): July 1st 1951.
Mwanzilishi
Serikali ya kikoloni ya Uingereza, iliweka chini ya Idara ya Maendeleo ya Jamii
Mtendaji Mkuu
Dr. Ayubu Rioba - ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC. Aliteuliwa na Rais mwaka 2016. kabla ya kuteuliwa alikuwa mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano na Umma (SJMC). Ni mwandishi wa habari mtaalamu (aliwahi pia kufan
Mhariri Mkuu
Dr. Ayubu Rioba -angalia hapo juu
Watu wengine muhimu
Rais - anateua afisa mtendaji mkuu/Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi
Waziri wa Habari - anateua wajumbe wengine wa bodi.
Waziri wa Fedha -anathibitisha bajeti ya Mwaka ya TBC
Mawasiliano
Tanzania Broadcasting Corporation
P.O. Box 9191, Dar-Es-Salaam
Tel.: +255222860760
Fax: +255 222865577
E-Mail: info@tbcorp.org
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Isa katika soko
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Kiwango cha hadhira kwa mujibu wa ripoti ya viwango vya GeoPoll ya Redio & TV (Aprili – Juni 2018).
Muhtasari wa vyombo vya habari
Director of Radio Services, TBC (September 2018). Media Owner Monitor Questionnaire TBC.