This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-rsf.org/en/ retrieved on 2022/05/18 at 02:14
Reporters Without Borders (RSF) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Reporters without borders

TBC Taifa

TBC Taifa ni chaneli ya Redio ya Tifa ya asili ya Radio Tanzania Dar es Salaam kwa hiyo inachukua mamlaka ya asili ya utangazaji wa umma ambayo ni kupasha habari, kuelimisha na kuburudisha. Hata hivyo kutokana na kuanzishwa kwa vyombo vingine ndani ya TBC, burudani imepewa sehemu ndogo sana.

Kwa mujibu wa mahojiano na Director of Radio Services amesema kuwa 75% ya vipindi vyake ni vya habari na elimu na 25% tu ni burudani. Kwa hiyo malengo makuu ya TBC Taifa ni kuelimisha na kupasha habari kuhusu masuala makuu ya taifa kama vile Sera za Serikali, Dira ya 2025, mpango wa miaka mitano na ilani ya Chama tawala – CCM.

Kwa mujibu wa ripoti ya Tanzania Media Measurement ya GeoPoll, kwa takwimu za hadhira za robo mwaka ya pili ya 2018, TBC Taifa ina hadhira ya XX.XXX%  Kwa hiyo ni ya nne miongoni mwa vituo vyote redio, na Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC) ni radio maarufu sana.

TBC ni chombo cha umma cha utangazaji pekee Tanzania Bara. Ni shirika la umma lililoanzishwa mwaka 1992 kwa mujibu wa Sheria ya Mashirika ya Umma, kutoa huduma za utangazaji ya umma kwa njia ya redio na televisheni. TBC inamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusimamiwa na Msajili wa Hazina, idara ndani ya Wizara ya Fedha, yenye 100% ya hisa. Lengo la Serikali ni kutumia TBC kuongeza nguvu juhudi za Serikali katika kujenga Taifa. Hatimaye, serikali inatarajia TBC kuwa msemaji wake kuliko kutangaza kwa uhuru wake bila ya upendeleo

Miongoni mwa matokeo itakuwa ushughulikiaji wa vyanzo vya habari. TBC Taifa inatumia 70% ya hoja za viongozi/mamlaka kama vyanzo vya habari. Hali hii ilibainishwa na utafiti wa ubora wa Vyombo vya habari uliyogharimiwa na Baraza la Habari la Tanzania (MCT). Imedai pia kuwa, ni habari moja tu kati ya nne, ilikuwa na muundo bora. Vipindi vyake vinavyowalenga wananchi wa kawaida havifiki hata nusu, na matangazo mengi yanahusu 8% ya masuala ya siasa.

Taarifa muhimu

Isa za hadhira

XX.XX%

Aina ya umiliki

umma

Maeneo yanayofikiwa

Taifa

Aina ya maudhui

Maudhui huru

Uwazi hafifu

Upatikanaji wa taarifa za wamiliki kutoka kwenye kampuni/chaneli

3 ♥

Kampuni ya vyombo vya Habari

Tanzanian Broadcasting Corporation

Umiliki

Muundo wa umiliki

TBC Taifa inaendeshwa kinadharia na umma lakini kwa vitendo inaendeshwa na Tanzanian Broadcasing Corporation inayomilikiwa na serikali

Haki ya kuchagua

Taarifa zisizopatikana

Mmiliki Binafsi

100%
Kampuni ya vyombo vya Habari
Halisia

Maelezo yote

Mwaka wa kuanzishwa

Started as„Sauti ya Dar es Salaam” (The Voice of Dar es Salaam): July 1st 1951.

Mwanzilishi

Serikali ya kikoloni ya Uingereza, iliweka chini ya Idara ya Maendeleo ya Jamii

Mtendaji Mkuu

Dr. Ayubu Rioba - ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC. Aliteuliwa na Rais mwaka 2016. kabla ya kuteuliwa alikuwa mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano na Umma (SJMC). Ni mwandishi wa habari mtaalamu (aliwahi pia kufan

Mhariri Mkuu

Dr. Ayubu Rioba -angalia hapo juu

Watu wengine muhimu

Rais - anateua afisa mtendaji mkuu/Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi

Mawasiliano

Tanzania Broadcasting Corporation

P.O. Box 9191, Dar-Es-Salaam

Tel.: +255222860760

Fax: +255 222865577

E-Mail: info@tbcorp.org

www.tbcorp.org

Taarifa za kifedha

Taarifa ya Kifedha

Taarifa zisizopatikana

Faida za uendeshaji

Taarifa zisizopatikana

Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)

Taarifa zisizopatikana

Isa katika soko

Taarifa zisizopatikana

Maelezo ya ziada

Taarifa ya ziada

Kiwango cha hadhira kwa mujibu wa ripoti ya viwango vya GeoPoll ya Redio & TV (Aprili – Juni 2018).

Muhtasari wa vyombo vya habari

Director of Radio Services, TBC (September 2018). Media Owner Monitor Questionnaire TBC.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Reporters without borders
  • Funded by
    BMZ