This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-rsf.org/en/ retrieved on 2019/12/12 at 17:32
Reporters Without Borders (RSF) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Reporters without borders

Wadhibiti

Wadhibiti – Je, mhusikani nani?

Wakati mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) inasimamia vyombo vya utangazaji na vya kielectroniki , Idaya  ya Habari Tanzania (,MAELEZO) inasimamia  magazeti. 

Kampuni  zote za vyombo vya habari pia zinatakiwa kusajili lkama ilivyo kampuni nyingine yoyote – Wakala ya usajili wa Biashara na leseni (BRELA). 

Majukumu  hayafahamiki kwa uwazi TCRA inajukumu zaidi la  kufuatilia maudhui ya utangazaji wa mtandaoni. MAELEZO inajukumu la maudhuhi ya magazeti. Mgawanyiko huu wa majukumu hauko wazi. The Electronic  and Postal Communications (Maudhui ya Mtandao) Regulations 2018, inaeleza maudhui ni sauti data,  makala au taswira/ picha – wize tuli au zinazosogea. Matokeo yake inaelekea kuwa  magazeti ya mtandao yatasimamiwa na TCRA  wakati nakala za karatasi za gazeti  hilohilo zinasimamiwa na MAELEZO.

Vyombo viwili  hivyo si kama vinatofautiana  tu kwa mamlaka  yao bali pia  katika muundo wa kitaasisi, mamlaka ya utekelezaji. 

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) taasisi ya serikali inayojitegemea kwa kiasi Fulani . Ili anzishwa chini ya Sheria. Tanzania Communication Regulatory, 2003, kusimamia mawasiliano ya kielectroniki, huduma za Posta na usimamizi wa Spektramu ya masafa ya Taifa, Mamlaka hiyo imechukua kazi za Tanzania Communications, Commissions (TCC) ambayo imevunjwa na Tanzania Broadcasting Commision (TBC)

 • Mamlakainatoa, inaongeza muda na kufuta leseni za vituo vya redio na televisheni pamoja na watoa maudhui kwenye mitandao. Wakati mwingine, kwa mfano, wakati TCRA inapotoa au kufuta leseni kwa kipindi na waziri mwenye we kabla ya kuchukua hatua. 
 • Kamati ya maudhui ya TCRA inafuatilia masuala ya maudhui ya utangazaji , malalamiko kutoka kwa waendeshaki na watumiaji na maswala ya ufuasi wa maadili ya utangazaji. Waziri wa mawasiliano amateua wajumbe wa kamati . 
 • Kuanzia chombo cha utangazaji ni ghali.

Ada ya maombi ya  leseni ya redio yaanzia USD1000 mpaka 2000na ada ya leseni ya awali ni kuanzia USD 700 mpaka 20,000, kutegemea kundi la leseni (KItaifa, kimkoa, kiwilaya au kijamii) ada ya maombi ya TV inaanzia USD 1000 kwa ajili ya sehemu ya soko la jamuu hadi USD 5000 kitaifa , wakati leseni ya awali ni usad 500 kwa TV ya jamii na USD 3000 kwa TV ya taifa. Watangazaji wa umma hawalipi ada hiyo. 

Idara ya habari Tanzania (MAELEZO)

Idara ya habari Tanzania (MAELEZO) ni Idara katika wizara ya Habari, utamaduni, sanaa na michezo yenye jukimu la kuwaarifu wananchi kuhusu sera, programu na utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Tangu mwaka 2008 hadi sasa, idara ya habari Tanzania ipo chini ya Wizara ya haari , tamaduni, sanaa na michezo na sasa Dkt Hassan Abbasi kama Mkurugenzi. Mkurugenzi pia ni msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania chini ya media services Act, 2016, mkurugenzi wa Idara ya habari inatoa leseni kwa magazeti na ana mamlaka ya kukataa au kufuta leseni iwapo maombi hayakidhi masharti au leseni inakiuka masharti ya lseni. Leseni ya kumiliki f gazeti inahitaji ada ya Tsh 1,000,000 na dhamana ya Tsh. 100,000,000/= . Magazeti ni lazima yasajiliwe kila mwak wakati kampuni za nchini au watu binafsi hawana ukomo wa kumiliki hisa za kumiliki chombo cha habari, kampuni, ya nje hawezi kuwa na zaidi ya asilimia 49 katika kampuni ya vyombo vya habari ya Tanzania . 

 

 

 • Project by
  Media Council of Tanzania
 •  
  Reporters without borders
 • Funded by
  BMZ